Swala la kujiendeleza kimasomo, kuanzisha biashara au hata kutapata kazi wakati mwingine sio jepesi. Hasa pale unapohangaika kutafuta ada, nafasi ya chuo, mtaji au ujuzi wa biashara au hata kazi inayofaa ili kutimiza ndoto na kulisha familia, changamoto hulinganishwa na kupanda mlima mkali. Ni kweli, wakati mwingine wapo ndugu na jamaa kufariji au kuwezesha kwa namna moja au nyingine. Wakati mwingine pia unalazimika kuanza kwa kiwango cha chini na kutumia rasilimali ulizonazo ili kujiendeleza, hata kama hali hairidhishi. Katika juduhi zote za kumudu changamoto hizi, tunakutia moyo usonge mbele. Iwapo unajiona uko katika njiapanda na unahitaji msaada katika kumudu changamoto zako, jisikie huru kuwasiliana nasi. Katika kipindi cha miezi mitatu ijayo hatuzatoza gharama yoyote, maana mafanikio yako ni kipaumbele chetu. Tena, huduma yetu haishii kwenye ushauri tu, bali tunakupatia mwongozo na tutashirikiana nawe mpaka utakapofanikisha malengo yako.
Kheri ya Siku Kuu na Mwaka Mpya
Mpendwa msomaji,
kwa maneno haya machache ninapenda kukushukuru kwa kusoma machapisho yetu na kukutakia kheri ya siku kuu na mwaka mpya wenye afya na baraka katika kutimiza njozi na mipango yako.
Iwapo ni mara yako ya kwanza kuingia katika ukurasa huu, tafadhali jipatie wakati mfupi na kupitia machapisho yalioandikwa hapo chini. Tutafurahi kupokea maoni yako.
Machapisho haya yamelenga kutia moyo vijana katika safari yao ya kujiendeleza kimasomo na kiuchumi, na kuwahabarisha katika mada kadha wa kadha, k.v. namna ya kufungua biashara, vidokezo kuhusiana na namna ya kujiendeleza kielimu, kumudu mapato binafsi n.k. Iwapo kuna mada unayotamani tuiwasilishe hapa na inayoweza kuwa na manufaa kwa vijana, usisite kutuandikia. Pia usisite kujulisha wengine kuhusu tovuti/blogu hii ili pia hata wao waweze kufaidika.
Tunatarajia mwakani, tutakapokuwa na wasomaji wa kutosha, kufungua jukwaa la majadiliano (forum) kuhusiana na mada tunazihudumia katika tovuti yetu. Kwa taarifa zaidi kuhusu mada zetu, angalia hapa. Jukwaa hili husaidia wadau kubadilishana mawazo, kufahamiana, na kujitengenezea mtandao wa kusaidiana katika mada husika (kwa mfano fursa za mafunzo maalumu, upatikanaji wa kazi n.k.). Iwapo una shauku, jiskie huru kujiunga kupitia fomu hii. Tutakujulisha hatua zinazoendelea, na baada kupokea watu wa kutosha, tutalifungua jukwaa hilo la mawasiliano.
Nabaki kukutakia kila la kheri katika siku kuu na mwaka mpya, mapumziko mema ya shughuli na baraka tele katika kutimiza malengo mapya katika mwaka unaokuja.