Je, unalo wazo la biashara lakini unakosa nyenzo au msaada wa kitaalamu kulitekeleza? Katika dunia inayokumbwa na changamoto ya ukosefu wa ajira, vijana wanapaswa kuwa nguzo ya mabadiliko. Kwa kutambua hili, Consultation Center for Societal Nurturing (CCSN) imeanzisha mchakato wa kusaidia vijana kama wewe kufanikisha ndoto zao za kibiashara.
Lengo letu ni kuleta suluhisho la kudumu kwa tatizo la ukosefu wa ajira, si tu kwa kuwasaidia vijana mmoja mmoja, bali pia kwa kuhakikisha kuwa jamii kwa ujumla inanufaika. Tunajua kuwa kijana mwenye fursa ya kujiajiri anaweza kugeuka kuwa chachu ya maendeleo, si kwake tu bali pia kwa wale waliomzunguka. Hivyo, tunakuwezesha katika:
• Kupata sehemu ya mtaji wa kuanzisha biashara yako.
• Ushauri wa kitaalamu na maarifa yatakayokusaidia kusimamia biashara kwa mafanikio.
• Fursa ya kukuza mtandao wako wa kibiashara na kujifunza kupitia vijana wengine wenye mafanikio.
FURSA HII NI YAKO!
Huu ni wakati wa kuchukua hatua. Ikiwa unalo wazo la biashara, CCSN ipo hapa kukupa nguvu unayohitaji ili kulitekeleza. Tunakualika utume wazo lako la biashara pamoja na mpango kazi kwa barua pepe info@societalnurturing.com nasi tutawasiliana nawe kwa ajili ya hatua zaidi.
KWA NINI TUFANYE HAYA?
Sisi CCSN tunaamini kuwa kila kijana ana uwezo wa kuwa mshindi endapo atapewa nafasi na msaada sahihi pale anapohitaji kujikwamua kimaisha na kuiishi ndoto yake. Tunataka kuona kizazi kinachoongozwa na maarifa, ubunifu, na bidii, kikibadilisha hadithi ya ukosefu wa ajira na kuwa mfano wa mafanikio. Fursa ya kuinuana ni ya pekee, na tunaamini kuwa pamoja tunaweza kujenga jamii bora, yenye mafanikio na maendeleo endelevu.
USIKAIE HII NAFASI!
🌟 Wazo lako la leo linaweza kuwa biashara kubwa ya kesho.
🌟 Safari yako ya mafanikio inaanza na hatua moja – kutuma mpango wako kwetu.
🌟 Jiunge nasi na tufanye kazi pamoja kuleta mabadiliko makubwa.
Tutafurahi kupokea ujumbe kutoka kwako uwako.