CCSN imeanzisha mradi mdogo wa kukausha matunda na kuyauza kama kitafunwa cha asili (bila kuongeza sukari au kemikali) na hivyo kutengeneza ajira kwa vijana na kuepusha uharibiribifu wa matunda ya msimu, hasa maembe na mananasi. Baada ya kufanikisha zoezi la kukausha na kupata miitikio chanya kutoka kwa watu, tuko sasa katika utaratibu na maandalizi ya usajili wa biashara hiyo kupitia SIDO na TBS.
Kitafunwa hiki kimepata mwitikio mzuri kwa watoto na hata kwa watu wazima, kama kiburudisho, kionjo, kipoza njaa au kama zawadi kwa mtu. Pembeni na vitanfunwa tunavyovifahamu, kama vile karanga, korosho, bisi au bisukuti, sasa tumeongeza kingine kinachotokana na matunda yetu ya asili. Kama una shauku ya kujaribu bidhaa yetu, kushiriki katika biashara yetu au hata kutupatia maoni yoyote, karibu uwasiliane nasi.